Kumbukumbu ya Sheikh Muhammad Nassor (r.a)
Mwasisi wa Jumuiya Zawiyatul Qadiriya Tanzania
Innalillahi wa inna ilaihi rajiun. Kwa unyenyekevu na shukrani kwa Mwenyezi Mungu (S.W), Jumuiya Zawiyatul Qadiriya Tanzania inamkumbuka kwa heshima kubwa mwasisi wetu, Sheikh Muhammad Nassor (rahimahullah), aliyeanzisha jitihada za Jumuiya hii tangu mwaka 1980 hadi ilipopata usajili rasmi mwaka 1992.
Kwa miaka mingi, Sheikh aliongoza kwa hekima na uadilifu, akijenga msingi imara wa umoja wa Kiislamu ulio dhahiri hadi leo katika mikoa, matawi na vituo vya Jumuiya kote nchini Tanzania. Alilea vizazi vya wanafunzi na wanajumuiya kwa mafundisho ya kweli ya Tariqa Qadiriya, akisisitiza maadili ya Qur'ani na Sunna za Mtume Muhammad (S.A.W).
Kila mwaka, Jumuiya huadhimisha Hadhara maalum kwa kumkumbuka na kumuombea rehema, ushahidi wa upendo na heshima kubwa aliyoacha mioyoni mwa wanajumuiya wote alioutumikia kwa dhati.
Mwenyezi Mungu amrehemu Sheikh Muhammad Nassor, amlaze mahali pema peponi, na atujaalie sote kuenzi nyayo zake njema. Amin.